KUTOKA MAGAZETINI LEO 29/09/2015
Nape atumia muda wa kampeni kutukana
Nape atumia muda wa kampeni kutukana Jonas Mushi na Veronica
Romwald, Dar es Salaam MJUMBE wa Kamati ya Ushindi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye ametumia muda wote aliopewa kumnadi
mgombeaa urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli kumtukana mgombea urais
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayewakilisha Ukawa,
Edward Lowassa pamoja na viongozi wenzake. Katika mkutano huo
uliofanyika jana katika viwanja vya Samora mjini Iringa na kurushwa moja
kwa moja katika Kituo cha Star TV, Nape alitumia muda wake wote
kumtukana Lowassa pamoja na viongozi wa Chadema...
Published By: Mtanzania Lowassa apata mapokezi makubwa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga
Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa
shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye
Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo leo
Septemba 28, 2015. Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la
Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati
Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, leo Septemba
28, 2015. Waziri Mkuu...
Published By: ZanziNewsKipindupindu chatua Singida, yumo aliyetokea Dar
Wakazi 11 wa Manispaa ya Singida, wamelazwa kwenye kambi ya Mandewa
iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu, wakihofiwa kuugua
ugonjwa huo....
Published By: Mwananchi: Magufuli: Nakerwa na vigezo vya uzoefu kuomba ajira
Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo
atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi
wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu
ndio apatiwe ajira...
Published By: MwananchiNEC yajikanganya
*Mkurugenzi Tehama aondolewa * Maofisa watoa kauli tofauti NA
SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM MKURUGENZI wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (Tehama) wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Sisti
Cariah ameondolewa kwenye nafasi hiyo, imefahamika. Taarifa za uhakika
kutoka ndani ya NEC ambazo MTANZANIA ilizipata juzi na jana zimeeleza
kuwa mkurugenzi huyo ambaye ni mtu muhimu katika Tume ameondolewa katika
siku za karibuni huku kukiwa hakuna taarifa ya wapi alikohamishiwa
serikalini. Chanzo hicho cha ndani ya tume kimesema mkurugenzi huyo
ameondolewa siku tano zilizopita huku zikiwa zimesalia siku...
Published By: Mtanzania
Post a Comment: