KUELEKEA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI ,WACHUNGAJI 200, MAASKOFU 50 KUUNGANA NA JK
Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI
wa kiroho 250 wa madhehebu mbalimbali ya dini ya kikristo wamealikwa
kushiriki kwenye Tamasha la Amani Jumapili wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kati ya
viongozi hao 200 ni Wachungaji na 50 ni Maaskofu.
“Idadi
inaweza kuwa kubwa zaidi, lakini hadi sasa niseme hao ndiyo ambao tuna
uhakika nao watashiriki katika Tamasha la Amani Jumapili, ambapo mgeni
rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.
“Maandalizi
kuhusu tamasha yanaenda vizuri na nina imani Watanzania na wapenda
amani wote waliopo hapa nchini hata kama sio raia wa hapa watajitokeza
kwa wingi siku hiyo.
“Ni
tamasha ambalo dhamira yake ni kuomba kwa Mungu tuweze kupita kwa
usalama kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka
huu,” alisema Msama katika taarifa hiyo.
Tamasha
hilo lenye dhamira ya kuombea nchi amani kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa
Rais, Wabunge na Madiwani litahusisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za
Injili kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.
Baadhi
ya wasanii wa nje waliothibitisha kushiriki ni Sipho Makhabane, Sohly
Mahlangu wa Afrika Kusini, Sarah K wa Kenya, Ephraim Sekeleti wa Zambia
na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
anayeishi Kenya.
Baadhi
ya wasanii wa Tanzania watakaoshiriki ni Rose Muhando, Upendo Nkone,
John Lissu, Upendo Kilahiro, Boniface Mwaitege , kwaya ya St. Andrew ya
Dodoma na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.
Post a Comment: