JK AWAPA ZAWADI YA IDD MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ametoa zawadi
mbalimbali katika Mahabusu ya watoto walikinzana na sheria iliyopo
jijini Arusha
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kikwete,Katibu Tawala wa mkoa
wa Arusha,Addoh Mapunda amesema pamoja na kuwa watoto hao wanakabiliwa
na mashtaka ya kujibu lakini mheshimiwa Rais anatambua haki zao za
kushiriki na jamii kufurahia siku kuu hiyo ya kidini.
"Kama mnavyofahamu Rais Kikwete amekua na utamaduni wa kuwakumbuka
katika siku kama hizi ili nanyi mfurahie siku kuu hii,"alisema Mapunda.
Akipokea zawadi hizo Meneja wa Mahabusu hiyo,Mussa Mapua amesema imekua
ni faraja kwa kiongozi wa nchi kuwakumbuka na kuomba taasisi nyingine na
watu binafsi kuiga mfano huo na kumtakia Rais Kikwete mapumziko mema
anapojiandaa kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake.
Post a Comment: