Wednesday, 30 September 2015




Kumekua na staili mpya ambao ndugu zangu wale wa kijani na njano wamekua wakiwatambia wale wenzetu wa vidole viwili kwa wiki hii yote sasa wanaiita magufulika.
Suala lililozua gumzo leo mtaani ni pale wanapoonekana watu wenye haiba na hulka tofauti na ndugu yetu Magufuli wakisapoti na kushabikia staili hiyo mpya.
Huku mtaani ikiwa inaaminika ndugu pombe aliianzisha hii staili kudhibitisha uimara wake wa kutenda kazi na kutimiza yale anayoyaahidi likiwemo suala la uzembe kazini na mafisadi,lakini hapo hapo watu wanaonekana kushabikia sana ni sampuli ya wale wale ambao ni wafuasi wa mkwere,nikimaanisha watu wa maneno mengi ya sio na vitendo (wazembe ) na wapenda sana kunufaisha matumbo yao binafsi(mafisadi )
Kutokana na hili, swali tulilojiuliza wengi je magufuli naye ni mkwere!? na kama si mkwere hawa wanamsapoti ilhali wakijijua wao ni wafuasi wa mkwere wana mpango na ajenda ipi iliojificha !? kuna jamaa yetu mmoja yeye alienda mbali na kudai ndugu pombe hakua tayari kwa hii kazi na alikurupishwa ndio maana hana budi kua televisheni inayosubiri amri kutoka kwa muongozaji mwenye kiongozo.Na ndio sababu wafuasi wa mkwere wanajiamini hatowadhuru na kumshabikia
Mchangiaji mwingine ambaye alipita tu kutafuna kashata za jioni jioni yeye alisema kushabikiwa kwa magufulika staili na wafuasi wa mkwere ni matokeo ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa USEMBA (upungufu wa sera mbadala ) kwa wana kijani na njano.
Basi mada ilizidi pamba moto ikichochewa na vijisenti vichache vya malofa kupata gahawa na kashata,ndipo naye muhuza kahawa akahitimisha mada kwa kuchangia hili “watanzania wa leo wanajua sana kwenda na mitindo ya kisasa inayokuja kwenye soko,hivyo ukiwaletea magufulika wamo,ukiwambia wapige kazi wataitika ila na huwezi wabadilisha katika kile wanachokipenda zaidi ama walichokiamua, hata ukikishusha thamani watakitafuta (ulipo tupo) na kukithamini hicho chao”hivyo tuwaache wakwere wasapoti magufulika ila siku ya mnada wa tarehe 25 haitouzika sababu wengi wanaujua ulafi wa wakwere.
 Ndipo nami Nilipoamua kuondoka kuja huku kwenu nako kuwajulisha hekaya za mtaa  

Post a Comment: