BREAKING NEWZ MIKUTANONI : ACT Wazalendo kuanzisha benki kwa watu wa Kigoma
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kitashawishi uanzishaji wa Benki
ya Kijamii ya Watu wa Kigoma (Kigoma Community Bank) ili kuwawezesha
wafanyabiashara, wakulima na vikundi vya ujasiriamali kupata mikopo kwa
urahisi na riba nafuu.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema hayo
alipokuwa katika mikutano ya kampeni katika majimbo ya Kigoma mjini na
Buhigwe kuwanadi wagombea wa chama hicho ambao walisema kukamilika kwa
mpango huo kutainua uchumi na maisha ya watu wengi wa Kigoma na mikoa ya
jirani.
Suala la kuanzisha Benki ya Kijamii kwa Watu wa Kigoma sio jambo la
utani, ni mojawapo ya mikakati kumi ya chama chetu cha ACT Wazalendo
tunayotaka kuitekeleza endapo tutapata ridhaa ya kushinda urais pamoja
na viti vingi vya ubunge,†alisema Zitto
Ukienda Mkoa wa Kiliamanjaro utakuta Benki yao, Wilaya ya Mwanga
katika Mkoa wa Kilimanjaro, Mbinga mkoani Ruvuma na Mufindi iliyopo
Iringa kote huko kuna Benki za Kijamii za maeneo hayo, tunataka na sisi
Kigoma tuanzishe Benki yetu ili isaidie katika kukuza mitaji ya biashara
za watu ambao wamekuwa wakishindwa kupata mikopo katika benki na
taasisi nyingine za kifedha,†aliongeza.
Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa masikini nchini ikiwa ni pamoja na
mikoa ya Tabora, Singida na Lindi ambayo licha ya watu wake wengi kuwa
na kipato cha chini, imejikuta ikizalisha mazao mengi na kuliingizia
taifa fedha za kigeni kama vile tumbaku na kahawa ambayo yamekuwa
muhimili mkubwa wa uchumi wa nchi.
Alisema Mkoa wa Kigoma ambao una wakulima, wavuvi, wafanyabiashara na
wafugaji unahitaji mtaji wa shilingi bilioni moja ili kuanzisha benki
hiyo

Post a Comment: