Saturday, 26 September 2015


























Mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Mh. John Magufuli nae amejiunga rasmi katika kampeni inaondelea kufanywa na wafuasi wa chama chake,kupitia jopo la wasanii Tanzania ya NIMES'TUKA.amedhihirisha hilo leo mchana huu akihutubia mkutano wa kampeni mjini Shinyanga unaondelea hivi sasa.Katika kampeni zake za awali zote kila alipopita Magufuli alikua akiwaeleza watanzania kua amejenga barabara zenye urefu wa elfu 17 hivyo hata shindwa kuijenga Tanzania lakini leo hii akihutubia mkoani hapa amesema itakua ni dhambi kwa mungu na kumkosea heshima bosi wake kama atasema yeye amejenga barabara hivyo kuyakana maneno yote ya awali hapo nyuma aliyokua akiyanadi.
pamoja na hilo ambalo ameonesha kust'uka Mh Magufuli ameendelea na hotuba zake zilezile za siku zote ambazo ni dhahiri kuwa amemezeshwa mstari kwa mstari.

Post a Comment: