Wednesday, 23 September 2015

 
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii na wananchi wengine alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi  Mjini Korogwe ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwapokea baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika Korogwe. Jumla ya wanachama 25 walijiunga na CCM katika mkutano huo.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
Baadhi ya wasanii waigizaji, Wema Sepetu (kulia) na Bibi Mwenda wakizungumza na WanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kuwashawishi waichague CCM kutokana na mazuri mengi iliyowafanyia wasanii.
Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (katikati) katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza uliofanyika Lushoto Jimbo la Mlalo. Kulia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza  viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.

Post a Comment: