BENKI YA DUNIA: TANZANIA YAONGOZA DUNIANI KUTOA HUDUMA ZA PESA KWA SIMUTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TANZANIA
ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma za pesa, kutoa mikopo na kutoa
riba kwa kutumia mawasiliano ya simu, Benki ya Dunia imesema na kuongeza
kuwa Tanzania ni moja ya masoko makubwa zaidi duniani ya kutoa huduma
ya fedha kwa njia ya simu.
Benki
hiyo ya Dunia pia imesema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa
kiwango cha juu katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(ICT) ikilinganishwa na nchi nyingine duniani na kulingana na uwezo
wake.
Benki
hiyo pia imesema kuwa nchi jirani ya Kenya inaongoza kwa kutuma pesa
kupitia mfumo wa M-Pesa katika eneo ambalo miaka michache iliyopita
lilikuwa eneo la kujidai la nchi tajiri tu duniani.
“Huu ni mfano kutoka Afrika ambao unaweza kuigwa na nchi zote duniani,” amesema
Profesa Kaushik Basu, Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia (WB) wakati
akiwasilisha kwa ufupi tu yaliyomo katika Ripoti ya Benki hiyo ya World
Development Report ambayo itatolewa hivi karibuni.
Profesa
Basu alikuwa anazungumza jana, Jumatatu, Septemba 28, 2015 kwenye
Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliozungumzia Hali ya Enzi za Digitali (Digital
Age) uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa ni
sehemu ya majadiliano kuhusu Malengo ya Maendeleo Mapya (SDG’s) ambayo
yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) ambayo muda
wake wa utekekezaji wa miaka 15 umefikia mwisho mwaka huu.
Akizungumza
katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Estonia Mheshimiwa
Toomas Hendrik Ilves na Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Kim,
Profesa Kaushik alisema:
“Tuko
katikati ya mapinduzi makubwa ya teknolojia, ambayo athari zake bado ni
ngumu sana hata kubashiri. Na hizi ni shughuli ambazo miaka michache
iliyopita zilikuwa hata hazina jina, lakini sasa inteneti na teknolojia
ya digitali inabadilisha maisha ya kijamii na kisiasa ya binadamu,” alisema Profesa Basu.
Aliongeza: “Chukulia
takwimu hizi – kuna kiasi cha utafuta habari kwenye google kiasi cha
bilioni 4.2 kwa siku moja, kila sekunde watu wanatuma tweet 6,000 na
rekodi ilikuwa Agosti mwaka 2013 wakati zilipotumwa tweet 143,199 kwa
sekunde wakati ilikuwa inaonyeshwa filamu moja ya sanaa.”
Aliongeza: “Mfumo
wa uwekaji na utumaji pesa wa M-Pesa katika Kenya sasa unashindana na
mifumo ya siku nyingi ya nchi matajiri duniani. Kila watu wazima 1,000
kuna akaunti 700 katika Kenya ikiwa ni ongezeko 103 kutoka mwaka 2013.”
“Jirani
na Kenya kuna mfano mwingine wa mafanikio makubwa zaidi duniani katika
nchi jirani ya Tanzania. Tanzania imewekeza sana katika ICT na katika
mfumo wa kuhamisha na kusambaza fedha. Sasa Tanzania ni soko kubwa zaidi
duniani la kutuma fedha kwa njia ya simu,” alisema Profesa Kaushik.
Aliongeza: “Tanzania
sasa ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma ya pesa, kutoa mikopo na
kutoa riba kwa njia ya simu. Hii ni mifano ambayo nchi zote duniani
zinaweza kuiga kutoka Afrika.”
Wakati
huo huo, Rais Kikwete leo, Jumanne, Septemba 28, 2015, amekutana na
kufanya mazungumzo na Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima wa Uholanzi, Mke
wa Mfalme Willem-Alexander kuhusu jinsi gani ya kuzidi kuisaidia
Tanzania kuongeza kasi yake katika kuboresha huduma za pesa kupitia ICT.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Septemba, 2015

Post a Comment: